Home Sports KIMATAIFA KAZI BADO HAIJAGOTA MWISHO

KIMATAIFA KAZI BADO HAIJAGOTA MWISHO

SIO utani kwenye kusaka ushindi kimataifa kazi ni ngumu ndani ya dakika zote 180 licha ya kuwa kila timu kufanya maandalizi mazuri.

Uwanja wa Mkapa, Simba walianza kazi yao kwa kupata ushindi dhidi ya Wydad Casablanca kisha mchezo unaofuata utakuwa ugenini.

Hakika kwa ushindi wa mchezo wa kwanza Simba mnapaswa pongezi huku mkitambua kuwa mna kazi ugenini.

Haitakuwa kazi nyepesi bali ni ngumu kwa kila timu kupata ushindi kutokana na maandalizi na uhitaji wa kila timu kupata ushindi.

Makosa ambayo yamefanyika kwenye mchezo wa kwanza ni muhimu kufanyia kazi huku wachezaji wakiongeza umakini kwenye mchezo wa kukamilisha robo fainali ya pili ugenini.

Kikubwa ni kufanya jitihada kwenye dakika 90 zilizobaki kwenye anga za kimataifa ili kufungua ukurasa wa kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali.

Mida ya malisho kwa wachezaji ni sasa katika kufanya maandalizi ya mwisho kwa kuwa kila mmoja ana kazi yake kwenye kusaka ushindi.

Yanga kete ya ugenini ambayo ilitarajiwa kukamilishwa jana ni mwanzo wa kusaka ngwe ya pili kusaka hatua ya kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali.

Wale ambao watakuwa mbali ya Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa marudio waendeleze dua kwa ajili ya Yanga kupata ushindi na wale ambao watakuwa karibu ni muda wao kujitokeza kuishangilia timu kwa shangwe.

Ushindi ambao wameupata ugenini ni muhimu kuendelea kuulinda kwenye mechi ya pili kukamilisha hesabu za kutinga hatua ya nusu fainali.

Wachezaji kazi ni kwenu kwa kuwa muda uliobaki hautoshi kupoteza ziadi ya kutumia kwa umakini katika kusaka ushindi na inawezekana.

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU
Next articleBEKI YANGA AWEKA REKODI YAKE KIMATAIFA