Home Sports BEKI YANGA AWEKA REKODI YAKE KIMATAIFA

BEKI YANGA AWEKA REKODI YAKE KIMATAIFA

BEKI mzawa Bakari Mwamnyeto kwenye anga la kimataifa ana pasi mbili kàtika Kombe la Shirikisho Afrika.

Pasi zote mbili alitoa akitumia mguu wa kulia nchini Nigeria ubao ulisoma Rivers United 0-2 Yanga.

Pasi zote alitoa kipindi cha pili ambapo moja ilikuwa nje ya 18 na moja ndani ya 18.

Pasi hizo mbili mtupiaji alikuwa ni Fiston Mayele ambaye anafikisha mabao 50 ndani ya Yanga katika mashindano yote.

Katika anga za kimataifa Mayele ametupia jumla ya mabao matano akiwa ni kinara.

Ikumbukwe huo ulikuwa mchezo wa robo fainali ya Kwanza, hitimisho Uwanja wa Mkapa.

Yanga imetanguliza mguu moja hatua ya nusu fainali ambapo mchezo wa robo fainali ya pili utakamilisha safari yao kuelekea kwenye hatua hiyo Afrika.

Previous articleKIMATAIFA KAZI BADO HAIJAGOTA MWISHO
Next articleJASHO LILIWAVUJA SIMBA DHIDI YA WYDAD