Home Sports IHEFU FUPA GUMU KWA SIMBA

IHEFU FUPA GUMU KWA SIMBA

KLABU ya Ihefu yenye maskani yake Mbeya ndani ya dakika 270 katika mechi tatu tofauti imekwama kusepa na ushindi mbele ya Simba.

Ilikuwa katika mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Mkapa ambapo ubao ulisoma Simba 1-0 Ihefu katika mchezo wa mzunguko wa pili ubao ulisoma Ihefu 2-0 Simba Uwanja wa Highland Estate.

Katika msako wa pointi tatu ndani ya  Ligi Kuu Bara Simba imeifunga Ihefu mabao matatu na kukomba pointi zote sita mazima.

Katika mchezo wa hatua  ya robo fainali Azam Sports Federation walipokutana Uwanja wa Azam Complex ubao ulisoma Simba 5-1 Ihefu.

Jumla katika dakika 270 Ihefu wametunguliwa mabao 8 huku wao wakiifunga Simba bao moja pekee na mtupiaji alikuwa ni Rafael Daud.

Ni Jean Baleke yeye katupia mabao matano kwenye mechi mbili, katika ligi kawatungua mabao mawili na katika Azam Sports Federation ni mabao matatu kawatungua wakati Simba ikitinga hatua ya nusu fainali.

Previous articleVIDEO;MO DEWJI AFUNGUKIA ISHU YA KUGOMEA BILIONI
Next articleHALI NI NGUMU KWELIKWELI TIMU ZIPAMBANE