HALI NI NGUMU KWELIKWELI TIMU ZIPAMBANE

KAZI ni ngumu wa kweli kwa sasa kutokana na ligi kuwa karibu na mwisho huku kila timu ikizidi kupambana kusaka ushndi ndani ya dakika 90.

Hakika mwendelezo wa baadhi ya timu kwenye uwanja sio mzuri kutokana na matokeo ambayo wanayapata kuwa hayana a furaha kwao. Licha ya hayo kutokea ni muhimu kuzidi kuwa na mipango makini uwanjani.

Tunaona kwamba kwa sasa ni lala salama ambayo inahitaji utulivu kwenye kutafuata matokeo kwa kuwa kila mchezaji anapenda kuona timu inashinda.

Ili ushindi upatikane ni muhimu kila mchezaji kutumia makosa ambayo yanatokea uwanjani pamoja na kufuata mbinu ambazo anapewa na benchi la ufundi.

Kwa sasa kila timu inahangaika kupata matokeo jambo ambalo awali halikuwa sawa kwa baadhi ya timu kutokana na kuchukulia masuala kwa hali nyepesi.

Kwa upande wa benchi la ufundi kwa sasa ni kuwapa mbinu bora wachezaji na kuwajenga kisaikolojia kwa matokeo ambayo yanapatikana.

Waamuzi pia ni muhimu kufuata sheria 17 za mpira ili watakapofanya maamuzi yaendane na kile ambacho kinasakwa na wachezaji.

Wengi wanapenda kuona matokeo mazuri na wachezaji nao furaha yao ni kupata matokeo mazuri hili lazima lifanikishwe kwa kila mmoja afanye kazi kwa umakini.

Mashabiki presha kubwa kwenye mechi za wakati huu ni lazima ziwekwe kando na kila mmoja atimize majukumu kwa wakati.