Home Sports HUYU HAPA KUPEWA MIKOBA YA ZIMBWE JR SIMBA

HUYU HAPA KUPEWA MIKOBA YA ZIMBWE JR SIMBA

WAKIWA na kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo dhidi ya Raja Casablanca mikoba ya nahodha msaidizi wa Simba, Mohamed Hussein Zimbwe Jr inatarajiwa kuwa mikononi mwa Gadiel Michael.

Zimbwe atakosekana kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa usiku wa kuamkia Aprili Mosi ikiwa ni mchezo wa hatua ya makundi kwa timu hizo mbili ambazo zimetinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa watakosa huduma ya Zimbwe kutokana na adhabu lakini wachezaji wengine wapo tayari.

“Tutakosa huduma ya nahodha msaidizi Mohamed Hussein lakini wapo wachezaji wengine wapo tayari kutokana na mbinu za mwalimu mwenyewe atakavyoamua kuanza.

“Tukiwa ugenini hatuna hofu kwani licha ya kwamba tumetinga hatua ya robo fainali mchezo wetu dhidi ya Raja Casablanca ni muhimu kupata matokeo mazuri tutafanya jitihada kubwa kupata matokeo,” alisema.

Gadiel alikuwa chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira tangu Machi 24 kwenye mazoezi yaliyoanza Uwanja wa Mo Simba Arena yupo kwenye msafara wa kwanza ambao unatarajiwa kuibuka Morocco kwa maandalizi ya mwisho.

Previous articleKIMATAIFA, MWENDO WA KUSAKA REKODI
Next articleMASTAA YANGA WALA KIAPO, CAF YAWAPA JEURI SIMBA