KIUNGO wa Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania Feisal Salum, Fei Toto amepewa program maalumu nchini Misri ili kurejea kwenye ubora wake.
Mazoezi hayo ni maalumu kwa ajili ya kumuongezea fitinesi kuelekea kwenye mchezo wa leo Machi 24 dhidi ya Uganda.
Stars ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo dhidi ya Uganda Uwanja wa Suez Canal, mjini Ismailia ukiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu Afcon.
Ipo wazi kwamba Desemba 2022 Fei Toto alitangaza kuvunja mkataba wake na Yanga na tangu wakati huo hajacheza mchezo wowote wa mashindano zaidi ya kufanya mazoezi binafsi.
Wachezaji wengine ambao wapo Misri kwa ajili ya mchezo huo ni pamoja na Mbwana Samatta ambaye ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo.
Tottenham Hotspur forward Dominic Solanke battles with Crystal Palace defender Maxence Lacroix during the English championship Premier League football match between Crystal Palace and Tottenham Hotspur on 27 October 2024 at Selhurst Park in London, England - Photo Ian Stephen / ProSportsImages / DPPI (Photo by IAN STEPHEN / ProSportsImages / DPPI via AFP)