KIUNGO wa Yanga na timu ya Taifa, Taifa Stars, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amepewa mazoezi maalumu kwa ajili ya kumuongezea fitinesi kuelekea kwenye mchezo wa leo dhidi ya Uganda.
Stars leo itakuwa mgeni wa Uganda kwenye Uwanja wa Suez Canal, mjini Ismailia nchini Misri ukiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu Afcon.
Kumbuka Desemba mwaka jana Fei Toto alitangaza kuvunja mkataba wake Yanga na tangu wakati huo hajacheza mechi yoyote ya mashindano zaidi ya kufanya mazoezi binafsi.
Gazeti la Championi ambalo lipo mjini hapa tangu Stars wanafika, lilimshuhudia Fei Toto akifanya mazoezi hayo na kwa mujibu wa kocha wa viungo, amesema kuwa kiungo huyo amekuwa akifanya mazoezi mara mbili zaidi ya wenzake ili kumtengenezea fitinesi kutokana na hali yake ilivyo.
Fei Toto alianza mazoezi hayo maalumu juzi Jumatano hadi jana ili kuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Uganda.
Hivyo sababu ya nyota huyo kupewa mazoezi hayo ni kumrejesha kwenye ubora wake ndani ya uwanja afanye kweli.
Tottenham Hotspur forward Dominic Solanke battles with Crystal Palace defender Maxence Lacroix during the English championship Premier League football match between Crystal Palace and Tottenham Hotspur on 27 October 2024 at Selhurst Park in London, England - Photo Ian Stephen / ProSportsImages / DPPI (Photo by IAN STEPHEN / ProSportsImages / DPPI via AFP)