MAYELE ANATUPIA KIMATAIFA MUSONDA NAYE YUMO

KWENYE hatua ya makundi akiwa amecheza mechi tano Fiston Mayele kajaza kimiani mabao matatu akiwa amewatungua Real Bamako mabao mawili na US Monastir bao moja.

Weka kando suala la uchoyo ambao ni asili ya washambuliaji wengi duniani Mayele ana pasi moja ya bao alitoa mchezo dhidi ya TP Mazembe Kwa mshikaji wake Tuisila Kisinda.

Mkali wa pasi za mwisho katika hatua hii ndani ya Yanga ni mwamba Kennedy Musonda akiwa nazo tatu zote kazitoa Uwanja wa Mkapa dhidi ya TP Mazembe,Real Bamako na US Monastir katupia kamba mbili.

Usisahau ni mzawa Mudhathir Yahya huyu ni nyota pekee ambaye amefunga katika hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika ndani ya Yanga ilikuwa dhidi ya TP Mazembe.

Mchezo ujao ni dhidi ya TP Mazembe ambapo Yanga itakuwa ugenini unatarajiwa kuchezwa Aprili 2,2023.