Home Uncategorized FULL SHANGWE LINAHAMIA UGENINI KIMATAIFA

FULL SHANGWE LINAHAMIA UGENINI KIMATAIFA

BAADA ya kutinga hatua ya robo fainali Yanga imeanza hesabu za mchezo wao ujao wa kimataifa dhidi ya TP Mazembe.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Aprili 2 DR Congo.

Ikumbukwe kwamba mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 3-1 TP Mazembe.

Kwenye mchezo huo ni Kennedy Musonda, Mudhathir Yahya na Tuisila Kisinda ambaye alianzia benchi walipeleka maumivu kwa wapinzani wao.

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa sasa wanapeleka shangwe DR Congo.

“Wanachama, Mashabiki na Wapenzi wa Yanga sasa tunapeleka shangwe la Kimataifa ugenini twende Congo kwa Tsh 700,000 tu! (Full Package),”.

Yanga imetoa gari kwa ajili ya safari kuelekea DR Congo kwa mashabiki kupata fursa ya kuhushudia mchezo huo ambapo watato tiketi bure kwa mashabiki watakaokuwa kwenye safari hiyo.

Previous articleSHINDA ZAIDI NA SLOTI YA BOOK OF ESKIMO MERIDIANBET KASINO
Next articleMAYELE ANATUPIA KIMATAIFA MUSONDA NAYE YUMO