AZAM FC KIBARUANI LEO

KIKOSI cha Azam FC chini ya Kocha Mkuu, Kali Ongala leo Machi 22 kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya JKU ya Zanzibar.

Huu ni mchezo maalumu kwa ajili ya maandalizi ya mechi zijazo za mashindano ambapo Azam FC inacheza Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Azam Sports Federation ikiwa imetinga hatua ya robo fainali.

Kwenye msimamo ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 47 ambapo mchezo wake uliopita wa ligi ilipoteza ugenini.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Highland ulisoma Ihefu 1-0 Azam FC na kuwafanya wayeyushe pointi tatu mazima.

Mchezo wao dhidi ya Gor Mahia ya Kenya uliotarajiwa kuchezwa Jumapili umeondolewa kwenye ratiba kutokana na sababu za kiusalama.

Tuzidi kuwaombea majirani zetu Kenya hali ya amani ipate kurejea kama zamani.