Home Sports BAO LA CHAMA LASEPA NA TUZO CAF

BAO LA CHAMA LASEPA NA TUZO CAF

BAO la Clatous Chama alilofunga kwa mpira wa pigo huru dhidi ya Horoya AC limechaguliwa kuwa Bao Bora la Wiki la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa michezo ya mzunguko wa tano.

Katika mchezo huo uliochezwa Machi 18,2023 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 7-0 Horoya.

Ilikuwa ni bao la mapema zaidi dakika ya 10 ambapo ni Jean Baleke huyu alichezewa faulo nje kidogo ya 18.

Kwenye mchezo huo Chama alifunga mabao matatu huku mawili akifunga kwa mapigo huru moja kwa pigo la faulo na lingine kwa pigo la penalti na lile moja la mwisho ilikuwa kwenye mwendo wa kawaida.

Ameingia kwenye orodha ya nyota wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika raundi ya tano aiwa na mshikaji wake Sadio Kanoute

Kura zinapigwa kwenye ukurasa wa Twitter wa CAF unaohusika na mashindano ya vilabu.

Pia wawili hawa wameingia kwenye kikosi bora wakiungana na nyota wengine kutoka Simba ambao ni Baleke na Shomari Kapombe.

Previous articleAZAM FC KIBARUANI LEO
Next articleSIMBA YABEBA VIUNGO WAWILI YANGA