Home Uncategorized CHAMA, NTIBANZOKIZA KWENYE MAJUKUMU MAPYA CAF

CHAMA, NTIBANZOKIZA KWENYE MAJUKUMU MAPYA CAF

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa mitambo yao yote ya kazi katika kikosi hicho ina kazi maalumu ya kufanya kuelekea kwenye mchezo wao dhidi ya Raja Casablanca ugenini.

Katika kundi C, Raja ni vinara wakiwa na pointi 13 kwenye mechi tano ambazo wamecheza hawajapoteza hata mmoja zaidi ya kuambulia sare moja na wameshinda nne.

Katika nne walizoshinda walikuwa mashuhuda Uwanja wa Mkapa ubao ukisoma Simba 0-3 Raja na kusepa na pointi tatu mazima.

 Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wachezaji wote wanatambua mchezo wao dhidi ya Raja utakuwa mgumu lakini lazima wafanye kweli.

“Tunakwenda ugenini mchezo wa mwisho baada ya kumalizana na Horoya na kupata ushindi mkubwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika sasa hao Raja wanafuata lakini tutakuwa ugenini.

“Wachezji wetu akina Clatous Chama, Saido Ntibanzokiza,Mzamiru Yassin, Sadio Kanoute hawa wanakazi kubwa ya kufanya ili kupata ushindi kwani hapo ndipo furaha yetu ilipo.

“Walitufunga Uwanja wa Mkapa kwa kweli walituchosha kwa kuondoka na furaya yetu basi nasi tunafanya maandalizi mazuri ili kupata ushindi kwenye mchezo wetu ujao,” amesema.

Chanzo Spoti Xtra imeandikwa na Dizo Click.

Previous articleKARIAKOO DABI MAKOSA YA KIBINADAMU YASIPEWE NAFASI
Next articleSHINDA ZAIDI NA SLOTI YA BOOK OF ESKIMO MERIDIANBET KASINO