KARIAKOO DABI MAKOSA YA KIBINADAMU YASIPEWE NAFASI

LIGI ya Wanawake Tanzania inazidi kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila timu kufanya kazi kubwa kusaka ushindi.

Unaona kwamba msimu huu mpaka sasa bado hakuna timu ambayo imejihakikishia nafasi ya kutwaa ubingwa kutokana na mipango kazi ambayo inafanywa.

Kwa sasa hilo ni jambo ambalo linapaswa kuendelea kupewa uangalizi na umakini hasa kwa kuboresha mazingira ya kuchezea.

Leo Uwanja wa Uhuru kunatarajiwa kuchezwa mchezo wa Dabi ya Kariakoo kwa upande wa Wanawake Yanga Princess dhidi ya Simba Queens.

Iwe ni mchezo wa mbinu kwa timu zote kucheza kwa umakini kusaka ushindi ndani ya dakika 90.

Wachezaji kwa muda huu uliopo ni muhimu kutambua kwamba ninyi ni walinzi wa wachezaji wenzenu uwanjani hivyo masuala ya kuumizana yasipewe nafasi.

Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza ipo wazi kwamba timu zote zilitoshana nguvu hivyo kwa sasa ni muda wa kuonyesha uwezo na kupambana kufikia malengo.

Kila mmoja ana nafasi ya kushinda ikiwa atatumia nafasi ambazo atatengeneza pamoja na kujituma kwa wachezaji kwenye kusaka matokeo.

Nidhamu nje ya uwanja na ndani ya uwanja ni muhimu hivyo ni muda wa kufanya kila kitu kwa umakini ili kufikia malengo.

Waamuzi wa mchezo wa leo nao ni muhimu kusimamia haki na sheria 17 za soka kwenye mchezo ili kupunguza malamiko na kupishana nay ale makosa ya kibinadamu.