Home Uncategorized IHEFU WAMEZIMA NDOTO ZA AZAM FC MAZIMA

IHEFU WAMEZIMA NDOTO ZA AZAM FC MAZIMA

MATUMAINI ya Azam FC kutwaa ubingwa kwa msimu wa 2022/23 yamezimwa mazima na Ihefu baada ya Machi 13,2023 kuwatungua bao 1-0 Uwanja wa Highland Estate, Mbeya.

Bao pekee la ushindi kwa Ihefu lilifungwa na Rafael Loth dakika ya 38 na kuwapoteza Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Kali Ongala.

Kuyeyusha pointi tatu ugenini kunaifanya Azam FC kusalia na pointi zake 47 baada ya kucheza mechi 25 wamebakiwa na mechi tano ambazo ni pointi 15 ambazo hata ikitokea wakashinda zote hawatawakuta vinara Yanga wenye pointi 65.

Ikitokea Azam FC akavuna pointi tatu kwenye mechi ambazo zimebaki atafikisha pointi 62 ambazo tayari zimeshafikiwa na Yanga hivyo vigezo vya kutwaa ubingwa vinawakataa mazima.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Ihefu, Azam FC waliwatungua bao moja Uwanja wa Azam Complex huku mtupiaji akiwa ni Prince Dube.

Ushindi wa Ihefu unawapa pointi tatu na kusonga mpaka nafasi ya sita kwenye msimamo wakiwa na pointi 33 kibindoni.

Previous articleUNATAKA USHINDI MKUBWA, NJOO HUKU | EXPANSE KASINO
Next articleYANGA V US MONASTIR LEO WAKUBWA KAZINI