Home Sports YANGA:US MONASTIR WATATUAMBIA WALITUFUNGAJE

YANGA:US MONASTIR WATATUAMBIA WALITUFUNGAJE

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa Waarabu watwaambia waliwafungaje kwenye mchezo uliopita kutokana na mipango kazi inayoendelea ndani ya timu hiyo.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi inashiriki Kombe la Shirikisho Afrika ipo hatua ya makundi inasaka pointi tatu ili kufikisha malengo ya kutinga hatua ya robo fainali ina pointi 7 kwenye kundi D baada ya kucheza mechi nne.

 Kituo kinachofuata ni dhidi ya US Monastri mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 19 wanakumbuka walipoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa mabao 2-0 ugenini.

 Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe alisema ni ngumu kuamini kuwa walipoteza mapema lakini kwa kuwa limetokea hakuna kitakachoweza kubadilika.

“Ukitazama tuliwafuata kwa malengo ya kupata ushindi ama pointi moja ugenini lakini wakatufunga sasa watatuambia waliwezaje kutufunga watakapokuja waache waje ili tumalizane nao mapema kabisa.

“Mbinu za benchi la ufundi la Yanga ni kubwa na zinaonyesha zinatoa majibu hasa kwenye mechi ambazo tunacheza kwa sasa uwanjani iwe ni za ligi ama zile za kimataifa wachezaji wanapambana kupata matokeo.

“Kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kuna raha kubwa kushinda ukiwa na mashabiki na Waarabu wakija lazima wakutane na kitu cha tofauti,” alisema Kamwe.

Chanzo:Spoti Xtra.

Previous articleSIMBA HAKUNA MUDA WA KUREMBA NI KAZIKAZI
Next articleSIMBA YATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA