SIMBA YATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

SIMBA inayonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira inatinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku ikionyesha kwa mara ya kwanza pira Dubai Uwanja wa Mkapa.

Ni ushindi wa mabao 7-0 Horoya uliopatikana baada ya dakika 90 mbele ya mashabiki waliojitokeza kwa wingi kushuhudia burudani hizo.

Mabao ya Clatous Chama ambaye katupia hat trick ilikuwa dakika ya 10, 36 kwa mkwaju wa penalti na dakika ya 70, Jean Baleke alitupia kamba mara mbili ilikuwa dakika ya 32 na 65.

Pia kiungo Sadio Kanoute alicheka na nyavu dakika ya 54 na 87 ambapo wamesepa na mzigo wa mama kwa kila bao kununuliwa kwa milioni tano.

Ni Baleke anakuwa mshambuliaji wa kwanza kufunga ndani ya Sima hatua ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 9 ikiwa nafasi ya pili ambazo hazitafikiwa na Horoya yeye pointi nne nafasi ya tatu huku Raja Casablanca wao wakiwa nafasi ya kwanza na pointi 13.