Home Sports HOROYA KUKUTANA NA JAMBO LA TOFAUTI KWA MKAPA

HOROYA KUKUTANA NA JAMBO LA TOFAUTI KWA MKAPA

ROBERTO Oliveira, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kila mchezo atafanya mabadiliko kulingana na mbinu za wapinzani wake anaokutana nao.

Timu hiyo ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa imetoka kushuhudia ubao wa Uwanja wa Manungu ukisoma Mtibwa Sugar 0-3 Simba.

Kwenye mchezo huo Oliveira alianza na washambuliaji wawili ambao ni Moses Phiri na Jean Baleke huku akimpa muda pia mshambuliaji wake Mohamed Mussa ambaye alitokea benchi kwenye mchezo huo.

Mchezo dhidi ya Horoya unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Machi 18 wanakumbuka walipoibukia Guinea Simba ilipoteza kwa kutunguliwa bao moja kwenye msimamo ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 6 vinara ni Raja Casablanca wenye pointi 12.

 Oliveira amesema kuwa wana kazi kubwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika mashindano ambayo sio mepesi lakini wanahitaji matokeo mazuri.

“Kila mchezo ambao tunacheza tunakuwa na mpango kazi maalumu ambapo tunahitaji kushinda na kufunga kwa kuwatumia wachezaji ambao tunao ukizingatia kwamba wengi wana vipaji na wanapambana kutafuta matokeo.

“Hakuna ambaye hatambui ubora wa wapinzani wetu ikiwa ni pamoja na Horoya lakini nao ni lazima tuwe na mpango kwa ajili ya kuwakabili na kuwabadilishia mipango kulingana na namna ambavyo tutakutana nao hasa kwenye sehemu ya mazoezi hapo ndipo tunafanyia kazi makosa yetu,” amesema Oliveira.

Previous articleBADO MUDA WA KUPAMBANA KUFIKIA MALENGO
Next articleUSHINDI UPO KWENYE MECHI HIZI HAPA LIGI YA MABINGWA