BADO MUDA WA KUPAMBANA KUFIKIA MALENGO

  MUDA wa kukamilisha kazi kwenye Ligi Kuu Bara ambayo ilianza kwa kasi unazidi kusogea kutokana na kila timu kubakiwa na mechi chache mkononi.

  Kila mmoja kwa sasa anapambana kuona namna gani atafikia yale malengo ambayo alikuwa ameanza nayo kwa msimu wa 2022/23 ambao unazidi kwenda kwa kasi.

  Hakuna ambaye anapenda kuona kwamba matokeo anayopaa yanakuwa tofauti zaidi malengo makubwa ni kupata pointi tatu kwenye ligi hilo lipo wazi.

  Ushindani ambao upo unafanya kila mmoja kupata kile anachostahili huku wachezaji nao wakipambana katika kutimiza majukumu yao hili ni jambo muhimu na inapaswa kuwa endelevu wakati wote

  Wale ambao walikwama kupata pointi tatu kwenye mechi zilizopita ni lazima wafanye kazi kubwa kufanyia makosa ambayo walifanya kwenye mechi zao zilizopita.

  Inawezekana kwa sasa kupata kilicho bora kutokana na uwezo wa wachezaji ambao wanao na kila mmoja anapenda kupata kilicho bora.

  Ipo wazi kuwa kila mmoja ana kazi kubwa kusaka pointi tatu kutimiza hesabu ambazo ni muhimu kuzikamilisha kwa sasa.

  Matokeo ya uwanjani yanatokana na mpangilio na mwanzo kabisa hapa tuliongea kwamba mipango inaanza mwanzo wa msimu mwisho ni kukamilisha hesabu na sio muda wa kuanza kuzinduka.

  Hakuna ambaye anapenda kuona matokeo mabaya lakini kinachotakiwa ni kuwa kwenye uimara ndani ya uwanja nan je ya uwanja ili wachezaji wazidi kuwa imara.

  Mzunguko wa pili ni lala salama kwa kila mchezaji pamoja na timu kupata kile ambacho walikuwa wanahitaji kufanya ndani ya uwanja.

  Hakika wachezaji ambao wamekwama kushindwa kuonyesha uwezo uwanjani wana kazi ya kujiuliza kwa wakati mwingine kwa ajili ya mechi zilizobaki.

  Benchi la ufundi na wachezaji ni muhimu kufanyia kazi makosa ambayo yamepita na hilo litawafanya wazidi kuwa imara.

  Kila mmoja anakazi kubwa kwa sasa kutimiza majukumu yake ni muhimu kwa sasa kukamilisha yale ambayo yanapaswa kufanyiwa kazi.

  Ugumu upo kwenye kila hatua na sasa lala salama inakazi kubwa kwani zipo ambazo zitashuka daraja na zipo ambazo zitapanda daraja.

  Zipo timu ambazo zimekuwa kwenye mwendo bora kwa sasa zina kazi ya kuendelea kuwa hivyo mpaka mwisho wa msimu ili wavune kile wanachostahili.

  Hakuna sababu ya kukata tamaa kwa sasa eti kwa kuwa mechi zimebaki chache pointi tatu ni muhimu kwenye kila mchezo na inawezekana kupata matokeo mazuri ambayo yatawapa furaha.

  Tunaamini kwamba kwa wakati huu wa lala salama kila mmoja atatimiza majukumu yake kwa umakini na kupata kile anachostahili kwenye ulimwengu wa mpira.

  Kwa wale ambao watakwama kupambana kwa hali na mali kwenye lala salama basi watakachokipata kitakuwa kiawahusu hivyo wanajukumu la kuendelea kupambana zaidi.

  Iwe ugenini ama nyumbani matokeo mazuri yanapatikana kikubwa ni kujipanga kwa umakini na kufuta makosa ambayo yamepita.

  Kurudia makosa kunafanya timu ikamwe kupata matokeo chanya hivyo ni wakati wa kuendelea kupambana kufikia malengo.

  Previous articleNABI KUMALIZA MCHEZO MAPEMA KWA WAARABU
  Next articleHOROYA KUKUTANA NA JAMBO LA TOFAUTI KWA MKAPA