Home Uncategorized MTIBWA YAKWAMA KWA SIMBA

MTIBWA YAKWAMA KWA SIMBA

MTIBWA Sugar kwa msimu wa 2022/23 imekwama kusepa na ushindi dhidi ya Simba kwenye mechi ambazo wamekutana ndani ya ligi.

Katika mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, timu hiyo ilpoteza mchezo huo.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 5-0 Mtibwa Sugar.

Hivyo mzunguko wa kwanza waliacha pointi tatu Uwanja wa Mkapa na kurejea kujipanga upya pale Manungu.

Walipokutana Uwanja wa Manungu Machi 11,2023 ilikuwa majanga kwao kwa kuacha pointi tatu.

Ubao ulisoma Mtibwa Sugar 0-3 Simba na kuwafanya Simba kukusanya pointi sita za Mtibwa Sugar.

Ni hat trick ilifungwa Uwanja wa Manungu mtupiaji akiwa ni Jean Baleke ambapo alifunga mabao yote kipindi cha kwanza.

Previous articleMANCHESTER UNITED YAGAWANA POINTI
Next articleYANGA YASEPA NA POINTI TATU ZA GEITA