BAADA ya sare ya kufungana mabao 2-2 katika mchezo wa Europa League raundi ya 16, Mikel Arteta amesema wapinzani wao watakwenda Emirates.
Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Jose Alvalade ubao ulisoma Sporting 2-2 Arsenal.
Mabao ya Sporting yalifungwa na Goncalo Inacio dakika ya 34 na Paulinho dakika ya 55 Kwa Arsenal ni William Saliba dakika ya 22 na Hidemasa Morita alijifunga dakika ya 62.
Mchezo wa pili unatarajiwa kuchezwa Machi 16, Emirates.
Mikel Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa matokeo ambayo wamepata ugenini sio mabaya kwani wana mchezo utakaochezwa nyumbani.
“Vijana wamefanya kazi kubwa lakini sio mbaya kuna kazi ambayo tutafanya kwenye mchezo ujao nyumbani,”.