Home International KIMATAIFA YANGA KUJA NA DOZI YAKIPEKEE

KIMATAIFA YANGA KUJA NA DOZI YAKIPEKEE

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa ushindi ambao waliupata dhidi ya TP Mazembe Uwanja wa Mkapaule ulikuwa ni kionjo.

Kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi Yanga ilishinda mabao 3-1 huku watupiaji wakiwa ni Kennedy Musonda, Mudhathir Yahya na Tuisila Kisinda.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa propaganda ambazo zinasemwa kuhusu timu hiyo kushindwa kufanya vizuri kwenye mechi za kimataifa itaonyeshwa kwa vitendo.
“Tumesikia kwamba kuna watu wanasema kuwa kwenye mechi ambazo tunacheza Uwanja wa Mkapa hatupati matokeo mazuri sasa mchezo wetu ujao tutafanya kweli.

“Tunataka Real Bamako wakiondoka Tanzania waende wakawaambie watu wa nchi yao kwamba wamekutana na Klabu yenye mashabiki bora Afrika”

Yanga inatarajiwa kuchezwa na Real Bamako Machi 8 Uwanja wa Mkapa lakini inatarajiwa kumenyana na Prisons Machi 3,2023 mchezo wa hatua ya16 bora Kombe la Shirikisho Uwanja wa Azam Complex,

Previous articleKAZI YA VIGONGO VYA YANGA MACHI
Next articleMAYELE AFICHUA MAGUMU YA CAF,PHIRI ATOA AHADI NZITO