UBAO wa Stade du 26 Mars, Mali kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika unasoma Real Bamako 0-0 Yanga.
Ni mchezo wa hatua ya makundi ambapo timu zote mbili zipo kwenye msako wa pointi tatu muhimu.
Wawakilishi kutoka Tanzania kwenye anga la kimataifa wameanza na washambuliaji wawili ambao ni Fiston Mayele na Kennedy Musonda.
Kiungo wa kazi ngumu Khalid Aucho amekwenda benchi baada ya kupata maumivu na nafasi yake ni Aziz KI ameingia.
Nyota huyo amepata maumivu baada ya kuchezewa faulo.