Home International GUARDIOLA AWANYOOSHA ARSENAL

GUARDIOLA AWANYOOSHA ARSENAL

KOCHA Mkuu wa Manchester City amekiongoza kikosi hicho kusepa na ushindi mbele ya Arsenal.

 Kwenye mchezo wa Ligi Kuu England licha ya kwamba walikuwa ugenini waliwashushia kichapo wenyeji wao na kusepa na pointi tatu mazima Februari 15,2023 na kuongoza ligi.

Baada ya zile dakika 90 za jasho ubao wa Uwanja wa Emirates pale kwa washika bunduki ulisoma Arsenal 1-3 Manchester City ikiwa ni furaha kwa wageni na huzuni kubwa kwa wenyeji.

Wale ambao walipeleka macho kwa City ni Kevin De Bruyne ilikuwa dakika ya 24 bao hilo halikudumu kwa kuwa washika bunduki waliamka na dakika ya 42 waliweka mzani sawa kupitia kwa penalti ya Bukayo Saka.

Kipindi cha pili, Pep ambaye amefanya kazi wa ukaribu na Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta akafumua nondo zote ambazo mwanafuzi wake alikuwa hazijui na alishangaa akitunguliwa mabao mawili.

Ni Jack Grealish dakika ya 72 na mwamba Haaland yeye alifunga ukurasa dakika ya 82 kwa kufunga bao la tatu likiwa lina maana ya kukamilisha pointi tatu na kuwafanya wafikishe pointi 51 ambazo zinamaanisha wanakuwa namba moja.

Arsenal ambao wamecheza mechi 22 bado wana kiporo mkononi kuwafikia City ambao wamecheza mechi 23 lakini wote wana pointi 51 kibindoni.

Previous articleSIMBA:MWARABU ANAKUFA NNE,YANGA YAIWEKEA MTEGO TP MAZEMBE
Next articleKILICHOWAMALIZA SIMBA, KILIWALIZA YANGA KIMATAIFA