Home Sports MALENGO YA SIMBA KIMATAIFA YAPO HIVI

MALENGO YA SIMBA KIMATAIFA YAPO HIVI

UONGOZI wa Simba umesema kuwa malengo makubwa kuelekea kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca ni kupata ushindi.

Ni Februari 18,2023 Simba ina kazi nzito ya kusaka ushindi dhidi ya vigogo Raja ambao wanaongoza kundi C wakiwa wametoka kuwatungua Vipers mabao 5-0.

Leo Februari 15,2023 Simba imefanya uzinduzi wa kampeni za hamasa kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Murtanza Mangungu, Mwenyekiti wa Simba amesema:”Dhumuni letu (viongozi) tunataka uwanja ujae. Kwa namna tulivyozungumza na wachezaji na benchi la ufundi wako tayari kutupa ushindi, “.

Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanyika Tegeta kwenye tawi la Home Boys.

Previous articleFEISAL NYOTA WA YANGA APATA AJALI
Next articleYANGA MACHO YOTE KWA TP MAZEMBE