UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya unaotarajiwa kuchezwa Februari 11,2023.
Mchezo huo ni wa hatua ya makundi ambapo ni msako wa pointi tatu muhimu kusaka nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano ndani ya Sima amesema kikosi kipo tayari na wanaamini watafanya vizuri kupata matokeo kwenye mchezo huo.
“Ukweli ni kwamba ushindani ni mkubwa na tunajua wapinzani wetu wanahitaji ushindi ambacho tutakifanya ni kuzidi kupambana kusaka ushindi.
“Inawezekana kufanya kazi kwa umakini hasa tukiwa ugenini na tuna amini tutakuwa na mchezo mzuri hivyo mashabiki wasiwe na hofu kila kitu kitakuwa sawa,” amesema.
Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye msafara wa kikosi kilichoelekea Guinea ni pamoja na Mzamiru Yassin, Sadio Kanoute, Moses Phir, Pape Sakho na Aishi Manula.