Home Sports HII HAPA REKODI TAMU ILIYOWEKWA NA JEMBE

HII HAPA REKODI TAMU ILIYOWEKWA NA JEMBE

NI Saleh Ally Mhariri, Mtendaji wa Global Publishers na mwandishi mahiri wa habari za michezo, ameweka rekodi ya kuwa mwandishi wa Habari wa kwanza Tanzania kuchaguliwa na FIFA kupiga kura ya kumchagua mchezaji bora wa FIFA wa Dunia.

Saleh Jembe amechaguliwa na FIFA kwa mara ya tatu wiki iliyopita, katika kitengo cha waandishi wa habari.

Hii inamfanya kuwa mwandishi wa Habari anayetambulika na kuaminika zaidi na shirikisho hilo kubwa zaidi la mchezo wa soka Kimataifa.

Hongera sana kwa jambo hilo kubwa katika kuipeperusha bendera ya Tanzania kwenye anga za michezo.

Previous articleBEKI WA KAZI SIMBA AREJEA
Next articleMERIDIANBET WANAKUPATIA ODDS NONO WIKIENDI HII