Home Sports NYOTA WA ZAMANI WA YANGA NA NAMUNGO USAJILI WAKE ACHA TU

NYOTA WA ZAMANI WA YANGA NA NAMUNGO USAJILI WAKE ACHA TU

MIONGONI mwa taarifa ambazo zilikuwa na sarakasi nyingi ni pamoja usajili wa nyota Mohamed Issa Banka kuibuka ndani ya Ruvu Shooting na kabla ya kuanza kucheza mkataba wake ukavunjwa.

Banka ambaye amewahi kukipiga ndani ya kikosi cha Yanga, Namungo na Mtibwa Sugar alipaswa kuwa ndani ya kikosi cha Ruvu Shooting kwenye mzunguko wa pili katika dirisha dogo

Nyota huyo alipewa dili la miezi sita na alikubali kusaini tatizo ikaja kwenye kuripoti kambini kuanza majukumu yake mapya kabla ya kuanza kucheza hata mchezo mmoja mkataba ukavunjwa.

Taarifa iliyotolewa na Ruvu Shooting, Januari 24,2023 ilieleza namna hii:”Uongozi wa Klabu ya Ruvu Shooting tumefikia makubaliano kwa pande zote mbili ya kuvunja mkataba kati yetu na mchezaji  Mohamed Issa Banka ambaye ameonesha utovu wa nidhamu wa kutowasili kambini tangu asajiliwe.

“Kwa sasa hayupo kwetu alipaswa kujiunga nasi dirisha dogo la usajili,”.

Nyota huyo alitambulishwa ndani ya Ruvu Shooting kuwa mwanafamilia mpya Desemba 31,2022 na kutangazwa kufikia makubaliano kuvunja mkataba Januari 14,2023.

Previous articleBALEKE APEWA SAA 48, SINGIDA BIG STARS YAISHTUKIA YANGA KWA GOMEZ
Next articleNAMUNGO YAMPA TABU KIPA WA KMC