Home Uncategorized YANGA YAONGEZA NGUVU ULINZI

YANGA YAONGEZA NGUVU ULINZI

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa unahitaji kuwa na ukuta imara ambao utakuwa unalindwa na makipa wenye uwezo mkubwa.

Kwenye dirisha dogo Yanga imemuongeza Metacha Mnata ambaye alikuwa anakipiga ndani ya Singida ig Stars ataungana na Diarra Djigui kipa namba moja, Aboutwali Mshery pamoja na Eric Johora.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa timu ili ipate ushindi inahitaji kuwa na wachezaji bora na wenye uwezo mkubwa.

Kesho Yanga ina kazi ya kusaka ushindi dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Mkapa.

Yanga ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 53 baada ya kucheza mechi 20 wakiwa wamepoteza mchezo mmoja ndani ya ligi.

Previous articleDODOMA JIJI 0-1 SIMBA
Next articleNYOTA BALEKE AIPA POINTI TATU SIMBA UGENINI