Home Sports BONANZA SEKTA YA UCHUKUZI USHINDANI MKUBWA

BONANZA SEKTA YA UCHUKUZI USHINDANI MKUBWA

NAIBU Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete alikuwa mgeni rasmi ambaye amezindua bonaza la Watumishi Sekta ua Uchukuzi.

Bonanza hilo limefanyika leo Januari 21,2023 katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Mlimani, Dar.

Michezo ya awali ilikuwa ni pamoja na kuvuta kamba, kukimbia kwenye magunia, mpira wa pete na mpira wa miguu pamoja na kukimbia na mayai.

Ni kwenye kuvutana kamba kati ya TASAC na Tazara, TASAC waliibuka wababe.

Katika mchezo wa mpira wa miguu TASAC 2-0 Tazara, TPA 2-0 Wizara na LATRA 1-1 Viongozi wa uchukuzi..

Hamad Mbegu, Mkurugenzi Msaidizi wa Sekta ya Uchukuzi amesema kuwa ni bonanza ambalo limewakutanisha wafanyakazi wote na kuwa pamoja.

“Kila mmoja amefurahi kuwa hapa ambapo wafanyakazi tunashirikiana na kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa katika majukumu yetu na kuboresha afya,”.

Previous articleVIDEO: ISHU YA MALI ZA SIMBA KUUZWA, BOSI ABAINISHA UKWELI
Next articleNYOTA HUYU WA DODOMA JIJI TARATIBU ANAKUJA