Home Sports IHEFU YATAMBULISHA MAJEMBE MAWILI MAPYA KUTOKA MSIMBAZI

IHEFU YATAMBULISHA MAJEMBE MAWILI MAPYA KUTOKA MSIMBAZI

NYOTA Nelson Okwa ambaye ni mali ya Simba kaibuka ndani ya kikosi cha Ihefu chenye maskani yake Mbeya, nyanda za juu Kusini.

Hakuwa na msimu mzuri ndani ya Simba ingizo hilo jipya kutokana na kushindwa kuonyesha makeke uwanjani.

Sababu kubwa ya kukwama kufanya vizuri ni kusumbuliwa na majeraha ambapo alitumia muda mwingi kupambania hali yake kabla ya kuanza kurejea mdogomdogo.

kwa mujibu wa Juma Mgunda ambaye ni kocha msaidizi wa Simba, hivi karibuni aliweka wazi kuwa sababu kubwa ya Okwa kutoonekana uwanjani ni kusmbuliwa na nyonga.

“Nimekuwa nikisema mara kwa mara kuwa Okwa hayupo fiti na anasumbuliwa na nyonga hivyo anapambania hali yake akitengamaa atarejea uwanjani,”.

Akiwa na Simba kwenye mechi za ligi ni mbili alicheza na kuyeyusha dakika 13 hakupata nafasi ya kufunga wala kutengeneza nafasi ya bao.

Mwingine ambaye yupo ndani ya Ihefu ni Victor Ackpan ambaye alikuwa akicheza pamoja na Okwa wapo hapo kwa mkopo.

Previous articleVIDEO:SEMAJI LA CAF LAMBACHAMBUA NYOTA MPYA/CHAMA NA NTIBA
Next articleISHU YA MORRISON MAAMUZI MAZITO, MASHINE MPYA SIMBA HADHARANI LEO