>

BOCCO ATUMA UJUMBE HUU KIMATAIFA

JOHN Bocco, Nahodha wa Simba, amesema hawatawaangusha Watanzania kwenye mashindano ya kimataifa kwa kuwa wapo vizuri na watapambana bila kuchoka. Simba ikiwa Kundi D la michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, leo Jumapili inatarajiwa kutupa kete yake ya pili mbele ya US Gendarmerie, mechi ikichezwa nchini Niger “Tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu na kila timu inahitaji ushindi nasi tutapambana kushinda. “Kwa upande wa ushindi hata…

Read More

AZAM FC BADO HAIJAFIKA KWENYE UBORA WENYEWE

KOCHA Mkuu wa Klabu ya Azam FC, Abdi Hamid Moalin, amesema bado hajaipata Azam anayoitaka na ubora wa kikosi chake kwa sasa hauzidi asilimia 65 hivyo bado jambo lao ni kusaka uimara kwa asilimia kubwa. Moalin amefunguka kuwa kuna levo ya ubora ambayo anahitaji kuiona kwenye timu yake, jambo ambalo bado analifanyia kazi kwa sasa…

Read More

SAKHO,BANDA WAMPA KIBURI PABLO KIMATAIFA

KUREJEA kwa Pape Ousmane Sakho ambaye aliumia katika mchezo dhidi ya ASEC Mimosas na kuimarika kwa kiwango cha winga Peter Banda, kumempa kiburi Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco kufanya vizuri katika mchezo wa leo Jumapili dhidi ya Union Sportive Gendarmerie Nationale ya nchini Niger. Simba leo Jumapili wanatarajiwa kumenyana na Union Sportive Gendarmerie Nationale katika mchezo wa pili wa Kundi D ndani ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa kwenye Dimba la Général Seyni…

Read More

NYOTA 7 YANGA WATIBUA MIPANGO YA KOCHA NABI

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema kuwa kukosekana kwa wachezaji wake zaidi ya saba katika kikosi chake, kunamvurugia mipango ya ushindi kuelekea michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC). Hiyo ni baada ya kuongezeka kwa majeruhi katika kikosi chake ambao ni Mkongomani, Jesus Moloko aliyeshindwa kumalizia mchezo…

Read More

SIMBA KUYAKOSA MABAO 11 MAZIMA LEO KIMATAIFA

WAKIWA na kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao ni wa makundi wawakilishi wa Tanzania, Simba watawakosa wachezaji wao watano ambao wamehusika katika kupatikana kwa mabao 11. Ni mchezo wa pili dhidi ya USGN ya Niger katika kundi D baada ya ule wa kwanza dhidi ya ASEC Mimosas kuweza kushinda kwa…

Read More

YANGA YAIVUTIA KASI MTIBWA SUGAR

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba upo tayari kwa ajili ya mchezo wao ujao wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar. Ikiwa ni namba moja katika msimamo na pointi 36 baada ya kucheza mechi 14 kituo kinachofuata ni Manungu. Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa hawana hofu na mchezo huo kwa kuwa maandalizi yapo…

Read More

MWENDO UMEUMALIZA SONSO,PUMZIKA KWA AMANI

KAZI ya Mungu haina makosa na tunapaswa kumshukuru kwa kila jambo ambalo linatokea kwenye maisha yetu ya kila siku kwa kuwa yeye ni muweza wa kila kinachotokea. Hakuna ambaye anaijua kesho hivyo kwa muda ambao upo kwa wakati huu kila mmoja anajukumu la kutimiza yale yanayofaa bila kuchoka. Wanafamilia,ndugu na jamaa katika kipindi hiki kigumu…

Read More

MSHAMBULIAJI WA SIMBA RUKSA KUIVAA YANGA

MTIBWA Sugar imethibitisha kuwa muda wowote kuanzia sasa, itaanza kumtumia winga wao raia wa DR Congo, Deo Kanda baada ya kila kitu kukamilika. Thobias Kifaru,Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kuwa walikuwa wanashindwa kumtumia nyota huyo kwa sababu kuna vitu kuhusu uhamisho wake vilikuwa havijakamilika ila kwa sasa kila kitu kipo sawa. Ikumbukwe kwamba nyota…

Read More

KOCHA AFUKUZWA,MRITHI WAKE KUANZA KAZI LEO

KICHAPO cha mabao 4-0 walichokipata Fountain Gate mbele ya JKT Tanzania katika mchezo wa Championship kimeotesha mbawa kibarua cha Ulimboka Mwakingwe aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo pamoja na kocha wa magolikipa Kibwana Nyongoli. Mbali na benchi la ufundi pia kandarasi za wachezaji wawili zimesitishwa ikiwa ni kwa Tony Kavishe na Khalifa Mwande kwa makubaliano…

Read More

REKODI YA DTB YATIBULIWA NA GREEN WARRIORS

BAADA ya kucheza mechi 16 bila kupoteza ambazo ni dakika 1,440 Klabu ya DTB ilinyooshwa bao 1-0 dhidi ya Green Warriors FC ambao waliweza kutibua rekodi hiyo katika mchezo wa 17 uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ilikuwa ni Februari 13 kwenye Championship. Wakati huu inajipanga kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya African Sports unaotarajiwa…

Read More

NABI AMPA KAZI HII MAYELE YANGA

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, ametoa majukumu mazito kwa wachezaji wa timu hiyo, akiwemo kinara wa mabao, Fiston Mayele kwa kuhakikisha wanatupia mabao ya kutosha katika mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar kwa lengo la kuendelea kuongoza ligi. Nabi ametoa kauli hiyo baada ya kurejea kwa ligi kufuatia kumaliza mechi za Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) huku wakiwa na kumbukumbu za matokeo ya suluhu katika mchezo wa mwisho dhidi ya Mbeya City kabla ya ligi kusimama kupisha Shirikisho. Yanga inaongoza ligi ikiwa…

Read More