Home Uncategorized BATO YA WATANI WA JADI KUPIGWA APRILI

BATO YA WATANI WA JADI KUPIGWA APRILI

BATO ya watani wa jadi ndani ya 2023 inatarajiwa kuwa ni Aprili 9 ndani ya Ligi Kuu Bara kwenye mzunguko wa pili wa 2022/23.

Mtanage wa kwanza wababe hawa wenye ngome zao pale Kariakoo ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 1-1 Yanga.

Watupiaji wote walitupia mabao yao ndani ya kipindi cha kwanza ikiwa ni pamoja na nyota Okra aliyekosa nafasi nyingi za wazi kuwatungua wapinzani wao.

Kwa upande wa Yanga ni kiungo Aziz KI alimtungua Aishi Manula kwa pigo la faulo akiwa nje ya 18 dakika ya 45 muda mfupi kabla ya mapumziko na mabao hayo yalidumu kwa muda wa dakika 90.

Awali mchezo huo ndani ya 2023 ulitarajiwa kuchezwa Februali kutokana na ratiba ya Kombe la Mapinduzi linaotarajiwa kuanza mapema Januari 2023 ratiba ikapanguliwa upya.

Mbali na hilo pia kuna mechi za Kombe la Shirikisho, Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na michuano ya Chan kwa timu za taifa.

Ni Aprili 9,2023 ngoma inatarajiwa kuchezwa baada ya ile ya Oktoba 23,2022 kila mmoja kusepa na pointi moja na bao moja.

Previous articleYANGA BILA FEI TOTO, KWA MIFUMO HII UNAPASUKA, SAIDO REKODI
Next articleWAKULIMA WAZABIBU WAFUNGA MWAKA KWA USHINDI