Home Sports MASTAA HAWA YANGA WAMEKALIA KUTI KAVU, MMOJA AONGEZWA KIKOSINI

MASTAA HAWA YANGA WAMEKALIA KUTI KAVU, MMOJA AONGEZWA KIKOSINI

KWENYE orodha ya mastaa wanaotajwa kuwekwa kwenye hesabu za kuondolewa ndani ya Yanga ni pamoja na Gael Bigirimana, Heritier Makambo,Tuisila Kisinda.

Ni majina mawili yataondolewa Yanga kwa wachezaji wa kigeni ili kupata wawili watakaoingia kwenye kikosi cha kwanza kwa sababu idadi ya nyota 12 inayohitajika imetimia.

Ni nyota wawili ambao wanatarajiwa kurejea kikosi cha kwanza cha Yanga ikiwa ni Yacouba Songne.

Nyota huyo ataanza kuonyesha makeke yake kwenye Kombe la Mapinduzi, Zanzibar Januari 2023.

Yanga imepangwa kundi B ikiwa na timu za Singida Big Stars na KMKM ambapo mabingwa watetezi ni Simba iliyopo kundi C ikiwa na timu za KVZ na Mlandege.

Azam FC wao wapo kwenye kundi A wakiwa na timu za Malindi na Jamhuri huku kundi D likiwa na timu za Namungo, Chipukizi na Aigle Noir.

Previous articleSTARAIKA MPYA AIKAMUA YANGA 700 M, BALAA, MANZOKI AUMIA CHINA
Next articleJEMBE LINALOWINDWA NA SIMBA, YANGA DILI LAKE LIMEFIKIA HAPA