Home Sports JEMBE LINALOWINDWA NA SIMBA, YANGA DILI LAKE LIMEFIKIA HAPA

JEMBE LINALOWINDWA NA SIMBA, YANGA DILI LAKE LIMEFIKIA HAPA

 Franis Kazadi aliyekuwa kwenye rada za mabosi wa Kariakoo dili lake linatajwa kubuma katika mitaa hiyo.

Nyota huyo raia wa DR Congo alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za kuibukia kati ya Simba na Yanga ambao walikuwa wanasaka saini yake.

Ni Simba walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kupata saini ya mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kukipiga ndani ya AS Vita.

Kwa sasa ni mchezaji huru baada ya dili lake ndani ya Klabu ya Al Masry kumalizika kwa nyota huyo aliyekuwa anatajwa kufuatiliwa na mabosi wa Yanga.

Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu wa Kazadi zinaeleza kuwa bado nyota huyo ana dili la kuibukia Bongo hivi karibuni.

“Kazadi ana dili la kuja Bongo ambapo awali ni Simba na Yanga walikuwa wanamuhitaji lakini inaonekana dili lake limekwama kwenye timu hizo hivyo anaweza kuibukia Singida Big Stars ama Azam FC,”.

Previous articleMASTAA HAWA YANGA WAMEKALIA KUTI KAVU, MMOJA AONGEZWA KIKOSINI
Next articleLIVERPOOL NDIO BASI TENA WACHAPWA NA CITY