Home Uncategorized KUUMIA KWA PHIRI SIMBA PASUA KICHWA USHAMBULIAJI

KUUMIA KWA PHIRI SIMBA PASUA KICHWA USHAMBULIAJI

KUUMIA kwa mshambuliaji tegemeo wa Simba, Moses Phiri kunalipasua kichwa benchi la ufundi kwa kuwa kila wakifikiria nani atapewa mikoba yao wanavurugwa.

Kibu Dennis uwezo wake kwa msimu wa 2022/23 umekuwa mbovu kwa kuwa kila anapopata nafasi maamuzi yake anayajua mwenyewe.

John Bocco nahodha wa Simba mwenye mabao matano bado kasi yake ile ya utupiaji haijarejea huku Habib Kyombo naye mambo yakiwa hayajawa mazuri kwake.

Mpango wa Simba kuboresha safu ya ushambuliaji hasa kwenye dirisha hili dogo inabidi uwape faida kuelekea mashindano ya kitaifa na kimataifa.

Phiri aliumia kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar walipotishana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

Nyota huyo katupia mabao 10 akiwa ametoa pasi tatu za mabao msimu wa 2022/23.

Nyota huyo anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja akitibu majeraha ya mguu aliyopata.

Previous articleDIAMOND PLATNUMZ – CHITAKI (OFFICIAL AUDIO & LYRIC VIDEO)
Next articleMATUMAINI YA UBINGWA KWA RANGERS YAPO