Home International KOCHA HISPANIA AKUBALI UWEZO WA BONO

KOCHA HISPANIA AKUBALI UWEZO WA BONO

 KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Hispania Luis Enrique ameweka wazi kuwa ubora wa kipa wa Timu ya Taifa ya Morocco ulikuwa mkubwa jambo ambalo lilimfanya afikirie kumbadilisha.

Hispania walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kupata ushindi lakini mambo yakawa tofauti walikwama kupata ushindi baada ya Morocco kushinda kwa penalti 3-0 Hispania ambao walikosa penalti tatu.

Ni historia kwa Morocco kutinga hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza ilikuwa mbele ya mashabiki 44,667 Uwanja wa Education City hayo yalitokea na ulimwengu wa michezo ukashuhudia maajabu hayo.

Morocco ilikuwa na nafasi ya kumaliza mchezo ndani ya kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao anayekipiga West Ham Nayef Aguerd ambaye alikosa nafasi ya kufunga na Hispania wao kwenye muda wa nyongeza ni Pablo Sarabia shuti lake liligonga mwamba na kufanya ngome ya Morocco kuwa salama.

Shujaa kwenye mchezo huo ambao ulichezwa kwa dakika 120 na ubao kusoma Morocco 0-0 Hispania ni kipa wa Timu ya Taifa ya Morocco Yassine Bounou ‘Bono’ ambaye aliokoa penalti mbili zilizopigwa na Carlos Soler na Sergio Busqets huku ile iliyopigwa na Sarabia iligonga mwamba jambo lililowapa nguvu Morocco kushinda na penalti ya ushindi ilipigwa na Achraf Hakimi.

Morocco itamenyana na Ureno kwenye hatua ya robo fainali ambao wameshinda kwa mabao 6-1 dhidi ya Uswisi kwenye hatua ya 16 bora.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumamosi ya Desemba 10,2022 huko Qatar.

Akizungumzia kuhusu nafasi yake ndani ya kikosi cha Timu ya Taifa ya Hispania baada ya kuondolewa kwenye hatua ya 16 bora,  Luis Enrique amesema: “Sijui kuhusu maamuzi yangu na hali yangu itakavyokuwa. Huu sio muda sahihi wa kuzungumzia uhusu wakati wangu ujao hii naona sio sawa kabisa.

“Mkataba wangu unakaribia kuisha unajua hilo lipo wazi nina furaha na timu ya taifa pamoja na watu ambao ninafanya nao kazi kwa sasa ninahitaji kufikiria kilicho bora kwa ajili yangu na taifa.

“Kuhusu penalti hilo ni jukumu langu kwa kuwa niliwachagua wapigaji penati watatu ambao wao walikuwa wana kazi ya kuchagua kufanya lakini wale wapigaji watatu wa mwanzo ni maamuzi yangu na wote wamefanya jambo moja, labda jambo ambalo nilikuwa ninafikiria ilikuwa ni kumtoa kipa Bono nje na kumuweka kipa mwingine,”.

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Morocco Walid Regragui amesema: “Walikuwa wanajua kwamba tuna kazi kubwa ya kufanya na walijitoa kwa moyo tulikuwa tunataka kujaribu na  kushinda kabla ya kufika kwenye hatua ya penalti ila tulikuwa tunajua kwamba kama tutafika huko tunaye kipa mzuri ambaye ni bora  duniani,”.

Previous articleURENO YATEMBEZA DOZI IKITINGA ROBO FAINALI
Next articleHIZI HAPA REKODI ZA NAMUNGO V YANGA