Home International NEYMAR AREJEA, BRAZIL WAPETA

NEYMAR AREJEA, BRAZIL WAPETA

NEYMAR Jr amerejea kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil na zali la ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Korea Kusini jambo ambalo limewaondolea hofu mashabiki wa timu hiyo ya taifa ambapo walikuwa wanadhani nyota huyo hatakuwa kwenye mechi zilizobaki baada ya kuumia.

Ushindi huo unawafanya Brazil kutinga hatua ya Robo Fainali Kombe la Dunia Qatar 2022 na inatarajiwa kukutana na Croatia kwenye mchezo ujao Desemba 9,2022.

Uwanja wa 974  Neymar alipachika bao dakika ya 13 kwa mkwaju wa penalti ambapo kinda Vinicius Junior huyu alifunga bao la ufunguzi dakika ya 7, Richarlison alitupia bao moja dakika ya 29  na Tolentino Coelho de Lime alipachika bao moja dakika ya 36.

Kurejea kwa Neymar ambaye alikuwa anapambania hali yake baada ya kuumia enka kwenye mchezo dhidi ya Serbia ambao ulikuwa ni wa ufunguzi kuliongeza nguvu kwenye mchezo huo ambapo aliwajulisha mashabiki kwamba amerejea kwa kufunga bao kwa mkwaju wa penalti.

Vinicius Junior ambaye alifunga bao la ufunguzi ameweka wazi kuwa ushindi huo ni maalumu kwa ajili ya Legend wa timu ya Taifa ya Brazil Pele ambaye kwa sasa anapambania afya yake ambapo yeye mwenyewe kupita mitandao ya kijamii aliweka wazi kuwa anaendelea vizuri na alifuatilia mchezo huo.

Richarlison kwenye mchezo huo alifunga bao moja na kufikisha mabao matatu kwenye Kombe la Dunia Qatar jambo ambalo limewapa furaha mashabiki na wachezaji wa Brazili.

Furaha kwa Korea Kusini ilipatikana kupitia kwa Seung-Ho Paik ambaye alifunga bao moja dakika ya 76 hivyo wameondolewa kwenye Kombe la Dunia wakiwa wameweka rekodi ya kuwafunga Brazili bao moja.

Previous articleMOSES PHIRI NA FISTON MAYELE NGOMA NZITO
Next articleHUYU HAPA MCHEZAJI BORA YANGA V PRISONS, ALIKIWASHA