UFARANSA HAO KOMBE LA DUNIA HATUA YA ROBO FAINALI

MSHAMBULIAJI wa Timu ya Taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe anakuwa mchezaji wa kwanza kwenye historia ya Kome la Dunia kufunga jumla ya mabao 8 kabla ya kugota kwenye miaka 24.

Mbele ya mashabiki 40,989 nyota huyo leo ametupia mabao mawili wakati ubao ukisoma Ufaransa 3-1 Poland, Uwanja wa Al Thumama.

Mbappe katupia mabao mawili dakika ya 74 na 90+1 huku lile la kwanza la ufunguzi wakilipata Ufaransa dakika ya 44 kupitia kwa Oliver Giroud.

Dakika ya 90+2 Poland walipata penalti kwa mara ya kwanza na kipa aliweza kuokoa mara ya kwanza pigo la Lewandoswki ambaye alipewa muda wa kurudia kwa mara nyingine kwa kuwa kipa alikuwa ametoka.

Ufaransa inakata tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali Kombe la Dunia kwa bao la Lewandoswki kwa mkwaju wa penalti.