Home Sports HAWA HAPA MASTAA WA YANGA WATAKAOIKOSA PRISONS

HAWA HAPA MASTAA WA YANGA WATAKAOIKOSA PRISONS

KUELEKEA kwenye mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons kuna baadhi ya nyota wa Yanga ambao wataukosa mchezo huo.

Kwa mujibu wa Cedrick Kaze, kocha msaidizi wa Yanga amesema kuwa wapo ambao wataukosa mchezo huo kutokana na sababu mbalimbali.

“Dickson Job ana adhabu hatakuwepo kwenye mchezo wa kesho, Jesus Moloko na Mayele hawajafanya mazoezi tutawaangalia kwenye mazoezi ya leo kama watatumika kwenye mchezo wa kesho.

“Bernard Morrison na Bakari Mwamnyeto wamerudi mazoezini lakini bado hawako vizuri asilimia mia moja,”.

Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 32 baada ya kucheza mechi 13 mchezo wake uliopita ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu ya Mbeya.

Previous articleCOASTAL UNION 0-0 SIMBA
Next articleSIMBA YAWATULIZA COASTAL UNION MKWAKWANI