Home International WAJAPAN WATUSUA KOMBE LA DUNIA BAO LAO SASA GUMZO

WAJAPAN WATUSUA KOMBE LA DUNIA BAO LAO SASA GUMZO

KUTOKANA na timu ya Japan kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya taifa ya Hispania, mchambuzi wa masuala ya michezo ameomba Shirikisho la Soka Duniani, FIFA kufanya uchunguzi kuhusu saka la mpira wa pasi ya mwisho ulioleta bao la ushindi.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Khalifa wakati ubao ukisoma Japan 2-1 Hispania watupiaji walikuwa ni Alvalo Morata kwa upande wa Hispania dakika ya 11 huku yale ya Japan yakifungwa na Ritsu Doan dakika ya 48 na lile lililozua utata lilifungwa na Ao Tanaka dakika ya 51.

Katika mchezo huo wa makundi Kombe la Dunia Qatar 2022 inaonekana kama kabla ya krosi kupigwa na Kaoru Mitoma kwa mchezaji mwenzake Ao Tanaka aliyeujaza mpira huo wavuni mpira ulikuwa umevuka mstari na kuwa kama upo nje ya eneo la kuchezea.

Tanaka alikamilisha kazi yake kwa kuujaza mazima mpira wavuni licha ya VAR kutazamwa bado ililikubali bao hilo lililoipa pointi tatu timu ya taifa ya Japan na inatajwa kuwa ilikuwa ni sawa na upendeleo kwa timu hiyo.

Ushindi wa Japan unaifanya imalize ikiwa ni namba moja kwenye kundi E baada ya kufikisha pointi 6 na Hispania inashika nafasi ya pili na pointi nne hizi zinatinga hatua ya 16 bora.

Licha ya timu ya taifa ya Ujerumani kushinda mabao 4-2 dhidi ya Coasta Rica wanagotea nafasi ya tatu wakiwa na pointi nne tofauti kwenye mabao ya kufunga na kufungwa na Hispania huku Coasta Rica ikigotea nafasi ya nne na pointi zake ni tatu hizi mbili Ujerumani na Coasta Rica safari imewakuta.

Mchambuzi huyo amesema:”Ujerumani sio taifa dogo kwenye mpira na kuna watu wasiozidi milioni 80 ambao kama hawaelewi suala hili wakisubiri kuona picha kama mpira ulikuwa sehemu ya mchezo au la.

“Kwa nini FIFA hawataki kueleza suala hili ambalo limeleta mkanganyiko? Ni muhimu kuweka usawa katika hili tafadhali,” amesema.

Previous articleINONGA ASHUSHA MASHINE MPYA SIMBA,MASTAA YANGA WAAPA
Next articleKIUNGO AOMBEWA ULINZI YANGA HUYU HAPA