Home International TIMU ZILIZOTOA WACHEZAJI WENGI KOMBE LA DUNIA

TIMU ZILIZOTOA WACHEZAJI WENGI KOMBE LA DUNIA

KUTOKANA na Kombe la Dunia la FIFA la 2022 linalofanyika Qatar kuanza karibia majira ya baridi, msimu huu umekuwa wa kitofauti ambapo ligi mbalimbali duniani zimesimama kupisha michuano hii mikubwa ya kimataifa.

Miaka ya nyuma, Kombe la Dunia limekuwa likichezwa punde tu ligi nyingi duniani zinapomalizika. Msimu huu hali imekuwa tofauti, ligi mbalimbali zilichezwa na sasa zimesimama kupisha michuano hii.

 Hali hii imesababisha klabu nyingi hasa zile kutoka ligi tano bora Ulaya kupoteza wachezaji wengi ambao wako kwenye majukumu ya kimataifa hivyo ili kuondoa utata na nguvu kazi kwenye vikosi ligi ambazo zina wachezaji wengi walioitwa timu za taifa zimesimama hadi pale michuano itakapomalizika.

Pamoja na kushirikisha nchi 32 bado kuna baadhi ya mastaa wa viwango vya juu ambao wanakosekana kama  Mohamed Salah, Erling Haaland, Jorginho, Sergio Ramos, Thiago na kadhalika watabaki nyumbani kuangalia kwenye runinga kutokana na timu zao kutofuzu au kutojumuishwa kikosini.

Klabu zinazopambana kuwania ubingwa kwenye ligi ndivyo ambavyo vimekuwa vikitoa wachezaji wengi zaidi kwenye Kombe la Dunia kuliko klabu ambazo zinajaribu kukwepa kushuka daraja.

Kuna wachezaji ambao walishaitwa kikosini na wakaanza maandalizi lakini wakaondolewa kutokana na kuumia siku chache kabla ya kuanza michuano.

Hapa kuna klabu ambazo zimetoa wachezaji wengi ambao wanaenda kushiriki michuano hiyo.

  1. Real Madrid (13)

Wametengeneza moja kati ya kikosi imara na bora Ulaya, hawa ndio Madrid ambao wamepeleka wachezaji 13 huko Qatar kuwakilisha mataifa yao.

Mastaa wao waliopo Qatar ni; Thibaut Courtois (Ubelgiji), Eder Militao, Rodrygo (Brazil), Dani Carvajal (Hispania), Antonio Rudiger (Ujerumani), Aurélien Tchouameni, Karim Benzema, Eduardo Camavinga (Ufaransa), Federico Valverde (Uruguay), Luka Modric (Croatia), Vinicius jr (Brazil), Eden Hazard (Ubelgiji), Marco Asensio (Hispania).

  1. Manchester City (15)

Kwa sasa hawako kwenye ubora wao sana kwani wameachwa kwa alama 5 dhidi ya vinara Arsenal kwenye Premier League lakini City ni moja kati ya klabu bora duniani kwa sasa wakiwa na mfungaji wao nyota Haaland lakini yeye haendi Qatar kwa kuwa taifa lake la  Norway halijafuzu.

Wachezaji wao walioitwa Kombe la Dunia ni; Manuel Akanji (Uswisi), Ederson (Brazil), Kevin De Bruyne (Ubelgiji), Ilkay Gundogan (Ujerumani), John Stones, Kyle Walker, Kalvin Phillips, Phil Foden, Jack Grealish (wote England), Joao Cancelo, Ruben Dias, Bernardo Silva (wote Ureno), Nathan Ake (Uholanzi), Aymeric Laporte and Rodri (Hispania).

  1. Manchester United (16)

Man U walikuwa kati ya timu iliyokuwa na usajili bora wakisajili majina makubwa na kila mchezaji waliyemsajili anawakilisha nchi kwenye Kombe la Dunia.

Wachezaji wao wanaoenda Kombe la Dunia wakitokea Man U: Kutoka Brazil wana Antony, Casemiro, Fred na Alex Telles (yuko kwa mkopo Sevilla), Christian Eriksen (Denmark), Raphael Varane (Ufaransa), Harry Maguire, Luke Shaw, Marcus Rashford (England), Diogo Dalot, Bruno Fernandes, Cristiano Ronaldo (Ureno), Facundo Pellistri (Uruguay), Tyrell Malacia (Uholanzi), Hannibal Mejbri (Tunisia), Lisandro Martinez (Argentina).

  1. Barcelona (16)

Barcelona wamebarikiwa kwa kuwa na wachezaji wenye vipaji vya juu nah ii imewafanya wapeleke nyota 16 huko Qatar huku nyota wao wengi wakiiwakilisha Hispania.

Nyota wao walioitwa timu za taifa ni;: Eric Garcia, Jordi Alba, Pedri, Gavi, Busquets, Ansu Fati and Ferran Torres (Hispania), Jules Kounde and Ousmane Dembélé (Ufaransa), Frenkie de Jong and Memphis Depay (Uholanzi), Raphinha (Brazil), Ronald Araujo (Uruguay), Ter Stegen (Ujerumani), Robert Lewandowski (Poland).

  1. Bayern Munich (17)

Bayern Munich imekuwa na msimu mzuri kwenye Uefa ambapo waliwapiga nje ndani Barcelona na kuwatupa Europa hawa jamaa wana wachezaji 17 huko Qatar, saba kati ya hao wakilitumikia Taifa la Ujerumani.

Mastaa wao walioitwa kikosini ni: Eric Maxim Choupo-Moting (Cameroon), Kingsley Coman, Dayot Upamecano, Benjamin Pavard (Ufaransa), Matthijs de Ligt (Uholanzi), Lucas Hernandez (Ufaransa), Sadio Mane (Senegal), Noussair Mazraoui (Morocco), Joshua Kimmich, Manuel Neuer, Thomas Müller, Jamal Musiala, Leroy Sane, Leon Goretzka, Serge Gnabry (wote Ujerumani), Josip Stanisic (Croatia), Alphonso Davies (Canada).

LIGI ZILIZOTOA WACHEZAJI WENGI

Premier League 136

La Liga 83

Bundesliga 76

Serie A 68

Ligue 1-       54

Previous articleSIMBA WAFANYA MAAMUZI MAGUMU, UNBEATEN YA YANGA KWISHAA
Next articleENGLAND HAO 16 BORA KOMBE LA DUNIA