>

DODOMA JIJI 0-1 YANGA, UWANJA WA LITI

IKIWA ugenini mbele ya Dodoma Jiji kwenye mchezo wa ligi Uwanja wa Liti, Yanga inaongoza kwa bao 1-0.

Bao pekee la uongozi ni mali ya Fiston Mayele ambaye amepachika bao hilo dakika ya 41 ya mchezo.

Pasi ya kwanza ya kiungo Tuisila Kisinda leo imeleta bao kwenye mchezo huo wenye ushindani mkubwa.

Dodoma Jiji wanakwenda vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa wamefungwa bao moja huku Yanga wakiwa mbele kwa bao moja.

Ni bao la 7 kwa Mayele kwenye ligi akiwa sawa na mzawa Sixtus Sabilo anayekipiga Mbeya City.