Home International VALENCIA AWEKA REKODI HII KOMBE LA DUNIA

VALENCIA AWEKA REKODI HII KOMBE LA DUNIA

MWAMBA Enner Valencia ameandika rekodi yake ya kufunga mabao mawili kwenye mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Dunia.

Wakati ubao wa Uwanja wa Al Bayt ukisoma Qatar 0-2 Ecuador ni Valencia alipachika mabao yote mawili ilikuwa dakika ya 16 kwa mkwaju wa penalti na dakika ya 31.

Bao lake la dakika ya tatu lifutwa baada ya VAR kuonyeshwa kuwa alikuwa ameotea.

Wenyeji Qatar wanaweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuanza kwa kupoteza mchezo wakiwa ni waandaaji wa mashindano hayo.

Previous articleMGUNDA KIBOKO YA NABI, ONGALA
Next articleAZAM FC MOTO NI ULEULE