Home Sports MGUNDA KUIFANYIA KAZI SAFU YA USHAMBULIAJI

MGUNDA KUIFANYIA KAZI SAFU YA USHAMBULIAJI

JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba amekiri kuwa wanatengeneza nafasi nyingi kwenye mechi ambazo wanacheza lakini tatizo lipo kwenye kuzitumia nafasi jambo ambalo linafanyiwa kazi.

 Safu ya ushambuliaji imetupia mabao 19 na kinara ni Moses Phiri mwenye mabao matano na pasi mbili za mabao.

Kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Singida Big Stars,Phiri alikosa nafasi ya kufunga dakika ya 7,20,44,52 na 71 huku Kibu Dennis akikosa nafasi ya kufunga dakika ya 47,51 na 66.

Mgunda amesema kuwa furaha ya mwalimu ni kuona timu inapata matokeo mazuri ambayo ni ushindi pale inapokuwa tofauti huwa hakuna anayefurahia jambo hilo.

“Kweli wachezaji wanapambana kusaka ushindi na wanacheza pia tunatengeneza nafasi nyingi lakini ambazo tunatumia ni chache hivyo hilo tunalifanyia kazi kwa ajili ya kupata matokeo kwenye mechi zetu zote katika eneo la mazoezi,” amesema.

Simba kibindoni ina pointi 21 baada ya kucheza mechi 10 kinara ni Yanga mwenye pointi 23 akiwa amecheza mechi 9.

Previous articleJUKUMU LA KULINDANA NI MUHIMU KWA WACHEZAJI
Next articleASTON VILLA WAINYOOSHA BRIGHTON