Home Sports JUKUMU LA KULINDANA NI MUHIMU KWA WACHEZAJI

JUKUMU LA KULINDANA NI MUHIMU KWA WACHEZAJI

WACHEZAJI wengi wamekuwa wakishindwa kukamilisha dakika 90 kwenye mechi ambazo wanacheza kutokana na kupata maumivu wakiwa kwenye majukumu yao.

Hii inatokana na mikimbio ambayo wanaifanya na wakati mwingine ni kutokana na mwili kutokuwa sawa unahitaji mapumziko yote yanatokea.

Lakini pia wakati mwingine wachezaji wanashindwa kukamilisha dakika zote 90 ama zile ambazo watapewa kutokana na kupewa maumivu na wachezaji wenzao ndani ya uwanja.

Hili halipo sawa ni muhimu wachezaji kutambua kwamba jukumu la kulindana linamuhusu kila mmoja na mchezo wa mpira hauhitaji nguvu nyingi bali akili.

Hata ikiwa mchezaji hayupo kwenye furaha kutokana na matokeo mabaya ambayo timu imepata bado kazi ni moja kusaka ushindi kwa umakini huku kila mmoja akiwa ni mlinzi wa mchezaji mwingine.

Uzuri ni kwamba mchezo wa mpira huwezi kuficha kila kitu kinaonekana na dakika 90 ni za jasho kwa kila mchezaji.

Kila kona ni msako wa pointi tatu kwa kila timu ambayo inaingia uwanjani muhimu kuwa makini kwenye kutafuta matokeo na inawezekana.

Jambo la msingi ni kila mmoja kutimiza majukumu yake kwa wakati ili kupata kile ambacho wanakistahili ndani ya uwanja hakuna namna nyingine.

Hii ina maana kwamba kila kitu kipo tofauti kuanzia kwenye maandalizi pamoja na utendaji kazi kwa wachezaji pamoja na mashabiki ambao wanajitokeza uwanjani.

Kumekuwa na mwendo wa kusuasua kwa timu ndani ya uwanja kwa wakati huu huku nyingine zikipata matokeo hilo lipo wazi hivyo kwa zile ambazo bado hazina matokeo mazuri ni muhimu kujipanga upya.

Kwa timu ambazo zimekuwa zikikwama kupata matokeo mazuri uwanjani haina maana ni mwisho kwao hapana ni lazimakujipanga upya na kufanya vizuri mechi zinazofuata.

Kwa wachezaji ambao wamekuwa wakionywa kwa kupewa kadi za njano kwa kucheza faulo mbaya kwa wachezaji wenzao hili linapaswa kufanyiwa kazi kwa mechi zijazo.

Kila mchezaji ni muhimu kwenye timu husika na anapopata maumivu kwa sabau ya kuumizwa na mchezaji mwenzake wakiwa kwenye mapambano hilo halipo sawa.

Matokeo yanatafutwa na kinacholeta matokeo ni maandalizi mazuri kwenye kila mchezo hilo ni jambo la msingi na muhimu kuzingatia.

Kwenye wachezaji ninapenda kutoa rai kwamba wakati wa kutimiza majukumu yenu tendeni haki kwa kufuata sheria zote 17 huku kila mmoja akiwa mlinzi wa mwenzake.

Ile kasumba ya kutumia nguvu nyingi kwa wakati huu muda wake umekwisha na nina amini kwamba wakati huu ni muda wa kutumia zaidi akili kuliko nguvu.

Kuharibiana kwa wachezaji kwa muda huu ni jambo baya na siku zote mchezo wa mpira si vita bali ni hesabu ambazo znapangwa na zikijibu matokeo yanaonekana.

Mpira una njia zake na kila kitu kinapaswa kufuatwa kwa wakati sahihi kwenye kazi ya kutimiza majukumu inawezekana na muda ni sasa.

Ipo wazi kwamba hakuna timu ambayo inaingia uwanjani ikiwa na hesabu za kupoteza mchezo kikubwa ambacho wanahitaji ni ushindi.

Hivyo basi kwa kuwa kila timu inahitaji ushindi ni muhimu kwa wachezaji kuamini kwamba ushindi unapatikana hata bila kuumizana.

Jambo la msingi ni kila mmoja kutimiza majukumu yake kwa ukamilifu akiamini kwamba mchezaji anapaswa kulindwa na sio kuumizwa ndani ya uwanja kisa msako wa ushindi.

Ugumu upo kila kona kwenye dakika 90 za kusaka ushindi inawezekana kwa kila mmoja kufanya kazi yake bila kumpa maumivu mwingine.

Matumizi ya nguvu yasipewe nafasi bali akili na kufanya kazi kwa kushirikiana hilo ni jambo la msingi na kila wakati iwe hivyo.

Mzunguko wa kwanza una mambo mengi lakini katika hayo lazima wachezaji wajue kwamba ni lazima wawe walinzi wa wachezaji wengine.

Kila kitu kinawezekana na ukweli ni kwamba licha ya mchezo wa mpira kuwa ni wa kutumia nguvu akili, pamoja na presha kuwa kubwa bado suala la usalama linawahusu wachezaji.

Hakika kwa sasa ni muhimu kila mmoja kutimiza majukumu yake akiwa na furaha huku akimlinda mwingine inawezekana.

Iwe ni Championship huku pia ni muhimu wachezaji kufanya kazi kwa umakini kwenye kutimiza majukumu yao.

Picha ambazo zimetumika kwenye makala haya hazina uhusiano wowote wa kuwahukumu wachezaji hao.

Tags # kitaifa

Previous articleMBUKINABE AANZA KAZI YANGA, MAJEMBE 4 YAMPA JEURI MGUNDA
Next articleMGUNDA KUIFANYIA KAZI SAFU YA USHAMBULIAJI