Home International MANE KUTIBIWA NA WAGAGA ACHEZE KOMBE LA DUNIA

MANE KUTIBIWA NA WAGAGA ACHEZE KOMBE LA DUNIA

INAELEZWA kuwa Senegal ipo tayari kuwatumia hata waganga wa kienyeji kuhakikisha nyota wao Sadio Mane anapona na kushiriki Kombe la Dunia ambalo linatarajiwa kuanza Novemba 20,kule Qatar.

Mane yupo kwenye hatihati ya kukosekana kwenye Kombe la Dunia baada ya hivi karibuni kuumia akiwa na Klabu ya Bayern Munich kwenye mchezo dhidi ya Werder Bremen.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa wa kwanza Mwanamke, Fatma Samoura amesema kuwa nchi yao itatafuta mbinu hata za ziada kuona Mane anapona kwenda Kombe la Dunia.

Samoura alisema kuwa kama matibabu ya kawaida yatashindikana basi watajaribu njia nyingine kuona kila kitu kinakwenda sawa.

“Tunaenda kutumia waganga wa kienyeji. Lakini sijui kama itawezekana, ila itabidi tufanye hivyo na matumaini yetu ni kuona miujiza inatokea,”.

Previous articleMFALME WA BETI NA KITOCHI WIKI HII, HAIJALISHI UNATOKA FAMILIA GANI
Next articleYANGA HII UNAPIGWA NJE NDANI