KOCHA Mkuu wa Chelsea, Graham Potter amesema kuwa Kepa Arrizabalaga ataukosa mchezo ujao dhidi ya Arsenal.
Mchezo huo ni wa Ligi Kuu England unatarajiwa kuchezwa Jumapili.
Sababu ya kipa huyo kuukosa mchezo huo ni kutokana na kusumbuliwa na majeraha.
Raia huyo wa Hispania ni chaguo la kwanza ndani ya Chelsea tangu Potter achukue mikoba ya Thomas Tuchel ila kwa sasa ana jeraha la mguu.
Wakati Chelsea ikicheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Dinamo Zagreb alikuwa ndani ya Uwanja wa Stamford Bridge lakini alionekana akiwa na magongo.
Kocha huyo kuhusu Kepa amesema:”Hapana hatakuwa sawa Jumapili. Ni tahadhari tu tunachukua lakini anaendelea vizuri,”.