Home Sports SIMBA YAPIGA 5G, MTIBWA MAJANGA KADI NYEKUNDU ZAWAPONZA

SIMBA YAPIGA 5G, MTIBWA MAJANGA KADI NYEKUNDU ZAWAPONZA

KIUNGO wa kazi ngumu ndani ya kikosi cha Simba, Mzamiru Yassin amerejea na nyota kali kwa kuwa miongoni mwa waliofunga mabao kwenye mchezo wa leo dhidi ya Mtibwa Sugar.

Baada ya dakika 90 kukamilika, ubao wa Uwanja wa Mkapa umesoma Simba 5-0 Mtibwa Sugar na kuifanya Simba kusepa mazima na pointi tatu.

Mzamiru alifungua pazia la mabao dakika ya 38 kisha mabao mawili yalifungwa na Pape Sakho dakika ya 48 na 90 huku Okra akifunga bao moja dakika ya 63 na Moses Phiri naye alitupia bao moja na kufikisha mabao matano.

Ilikuwa siku mbaya kwa Mtibwa Sugar kwa wachezaji wawili kuonyeshwa kadi nyekundu alianza Pascal Kitenge kish nahodha Issa Rashid.

Huu ni ushindi wa kwanza mkubwa kwa Simba chini ya Kocha Mkuu Juma Mgunda ndani ya ligi ambaye alitoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0dhidi ya Azam FC.

Salum Mayanga, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kadi mbili nyekundu zimewavurugia mipango ya kusaka ushindi pamoja na kuumia kwa kipa namba moja Faroukh Shikalo.

Previous articleMERIDIANBET SOKA BONANZA NI NURU KWA VIPAJI VYA VIJANA
Next articleTIKETI 10,000 MASHABIKI WA YANGA KUPEWA KUWAONA WAARABU