Home Sports DAKIKA 90 ZAKIBABE KARIAKOO DABI

DAKIKA 90 ZAKIBABE KARIAKOO DABI

DAKIKA 90 za Kariakoo Dabi kila mmoja kasepa na pointi moja baada ya sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Mkapa.

Simba walianza dakika ya 14 kupitia kwa Augustino Okra ambaye alionyeshwa kadi ya njano na mwamuzi Ramadhan Kayoko kwa kosa la kushangilia akiwa amevua jezi.

Ngoma iliwekwa usawa na Aziz KI kwa pigo huru dakika ya 45 akiwa nje ya 18 shuti ambalo lilimshinda mlinda mlango namba moja wa Simba Aishi Manula.

Ni sare ya kwanza kwa Kocha Mkuu wa Simba Juma Mgunda baada ya kubeba mikoba ya Zoran Maki.

Previous articleTAZAMA KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA SIMBA
Next articleILIKUWA SHOO SHOO, OKRA APEPEA NA MILIONI 300 ZA YANGA