LIVERPOOL YAKOMBA POINTI TATU ZA CITY

MOHAMED Salah mshambuliaji wa Liverpool amefunga bao pekee la ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Man City. Ni bonge moja ya mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa ambapo dakika 45 vigogo hao walikamilisha bila kufungana. Salah alipachika bao hilo dakika ya 76 lilitosha kuipa pointi tatu muhimu Liverpool. Sasa ni pointi 13 wanafikisha…

Read More

YANGA YAPOTEZA DHIDI AL HILAL KIMATAIFA

KIKOSI cha Yanga kimekwama kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika na sasa nguvu zao ni kwenye Kombe la Shirikisho. Kwenye mchezo wa leo dhidi ya Al Hilal walikubali kupoteza kw bao 1-0 Yanga. Ni bao la dakika ya 3 lilitosha kuwapa ushindi Al Hilal wakiwa nyumbani na kutinga hatua ya makundi. Mohamed Abdrahaman…

Read More

AL HILAL 1-0 YANGA

MCHEZO wa Ligi ya Mabingwa Afrika ni mapumziko. Al Hilal wanaongoza bao 1-0 Yanga ikiwa ni mchezo wa marudiano baada ya ule wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa kuwa Yanga 1-1 Al Hilal. Mtupiaji niMohamed Yusuph dakika ya 3 wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani. Bado wawakilishi wa Tanzania Yanga wana dakika 45 za kujiuliza…

Read More

SIMBA HAO MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

SIMBA imetinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya de Agosto. Mchezo wa ugenini Simba ilishinda kwa mabao 3-1 na leo Oktoba 16,2022 imeibuka na ushindi wa bao 1-0. Ushindi huo wakiwa nyumbani unawapa tiketi ya kufuzu hatua ya makundi chini ya Kocha Mkuu, Juma…

Read More

MOSES PHIRI AWATANGULIZA SIMBA KWA MKAPA

IMEWACHUKUA dakika 33 wachezaji wa Simba kusaka bao la kuongoza kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya de Agosto. Ni bao la Moses Phiri dakika ya 33 limefungua ukurasa wa uongozi kwa wenyeji Simba. Amepachika bao hilo akiwa kwenye uangalizi wa mabeki wa de Agosto akitumia pasi ya nahodha msaidizi Mohamed Hussein. Kwa…

Read More

NABI AJA KIVINGINE KUIKABILI AL HILAL

KATIKA kuhakikisha anapata matokeo mazuri ugenini dhidi ya Al Hilal, Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nasreddine Nabi, amepanga kufanya mabadiliko ya baadhi ya wachezaji kwenye kikosi cha kwanza kitakachocheza mchezo huo. Timu hizo zinatarajiwa kuvaana leo Jumapili kwenye Uwanja wa Al Hilal uliopo katika Mji wa Omdurman huko nchini Sudan katika mchezo wa marudiano. Katika…

Read More

HIKI HAPA KIKOSI CHA SIMBA V de AGOSTO

KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu Juma Mgunda leo Oktoba 16,2022 kinatupa kete yake kimataifa dhidi ya de Agosto ya Angola. Hiki hapa kikosi cha Simba kinachotarajiwa kuanza namna hii:- Aishi Manula Israel Mwenda Mohamed Hussein Joash Onyango Henock Inonga Sadio Kanoute Pape Sakho Mzamiru Yassin Moses Phiri Clatous Chama Okra

Read More

MAYELE:MSITUKATIE TAMAA INAWEZEKANA

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Kalala Mayele amewataka mashabiki wa timu hiyo kutokata tamaa kwani bado wanayo nafasi nzuri ya kufanya vizuri wakiwa ugenini. Nyota huyo amewaomba mashabiki wasiwakatie tamaa kwa kuwa bado wana nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi ya leo ambayo ni ya marudio. Yanga wameshindwa kutamba katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi…

Read More

MASTAA WATATU MSIMBAZI KUIKOSA de AGOSTO

MENEJA wa Habari na  Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa akili zao kwa sasa zinafikiria mchezo wa leo dhidi ya de Agosto ambao ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba chini ya Kocha Mkuu, Juma Mgunda ina kibarua cha kulinda ushindi wa mabao 3-1 ilioupata nchini Angola ili kuweza kusonga mbele katika hatua…

Read More

SIMBA YAPEWA PONGEZI NA YANGA KIMATAIFA

KASI waliyoanza nayo Simba katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika imemuibua Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe ambaye amekubali mziki wa watani zao hao na kuwatakia kila la kheri katika safari yao ya kusaka tiketi ya kufuzu hatua ya makundi kupitia mchezo wao wa marudiano dhidi ya C.D de Agosto ya Angola. Jumapili iliyopita…

Read More

MAYELE APEWA KAZI YA KUFANYA KIMATAIFA DK 90

FISTON Mayele mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Yanga anaingia kwenye dakika 90 za moto kushirikiana na mastaa wengine kupata matokeo ugenini kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal. Katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Oktoba 8, ubao uliposoma Yanga 1-1 Al Hilal ni Mayele alifunga kwa Yanga na kumfanya…

Read More

HAWA HAPA WATUPIAJI KIMATAIFA

 KWENYE anga la kimataifa rekodi zinaonyesha kuwa namba za wazawa kufurukuta ni finyu kutokana na wageni kutawala kila kona. Yanga na Simba wanaperusha bendera kwenye Ligi ya Mabingwa huku Azam FC kwenye Kombe la Shirikisho wao mchezo wao walipoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Al Akhadar ya Libya wana kazi ya kufanya mchezo wa…

Read More

HUYU HAPA AMETAJWA KUIPELEKEA SIMBA HATUA YA MAKUNDI

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa Kocha Mkuu Juma Mgunda wana imani naye atawapeleka hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kupata ushindi dhidi ya de Agosto ya Angola. Leo Simba inakibarua cha kusaka ushindi Uwanja wa Mkapa ikiwa na mtaji wa mabao 3-1 iliyopita ugenini dhidi ya de Agosto inahitaji kulinda ushindi huo…

Read More